Jumapili 9 Novemba 2025 - 11:00
Imam wa Ijumaa wa Najaf Ashraf Alilaumu Vikali Baraza la Usalama

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanchi, alisema: shambulio la hivi karibuni la Israel dhidi ya Lebanon na tamko rasmi la Israel, kwa mtazamo wa umma wa kimataifa ni ukiukaji wa maazimio ya kusitisha mapigano.

Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanchi, Imam wa Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika khutba za Ijumaa alizotoa katika Husayniyya Azam Fatimiyya ya Najaf Ashraf alisema: shambulio la hivi karibuni la Israel dhidi ya Lebanon na tamko rasmi la Israel kwamba shambulio hilo limefanyika kwa msaada wa Marekani, kwa mtazamo wa umma wa kimataifa ni ukiukaji wa maazimio ya kusitisha mapigano.

Aliongeza: jambo hili linaonesha kwamba siasa za dunia zinakabiliwa na upinzani wa wazi, kwani Baraza la Usalama linataka usitishaji wa mapigano, wakati ambapo Israel kwa msaada wa Marekani inakataa kwa ukaidi na inashambulia vikali kusini mwa Lebanon na Ghaza.

Imam wa Ijumaa wa Najaf Ashraf alisisitiza: maazimio ya Baraza la Usalama hayana tena thamani yoyote, na hili linamaanisha kwamba maazimio hayo hayamhusu mtoto mpumbavu (Israel), bali yanatuhusu sisi pekee.

Kuhusu Meya wa New York alisema: mada moto ya jana ilikuwa ni ushindi wa meya Muislamu wa New York na kauli yake hii: “Ikiwa Trump atafanya kosa, nitapambana naye,” na kauli ya Trump kwamba: “Nimepoteza sehemu ya mamlaka yangu.”

Khatibu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf aliendelea kusema: bila kujali nini ni sahihi au si sahihi, sisi tunaamini kwamba vita vinaendelea na Uislamu bila shaka utashinda na kufika njia yake.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha